Feature Image

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 lapiga Japani, onyo la tsunami latolewa

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.5 lapiga Japani, onyo la tsunami latolewa

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.5 lapiga kaskazini mwa Japani, na kusababisha mamlaka kutoa onyo la tsunami la mawimbi ya hadi mita 3 (futi 10).

Tetemeko hilo lilitokea Jumatatu katika maji ya mkoa wa Iwate kwenye pwani ya Pasifiki ya Japani, kulingana na Shirika la Hali ya Hewa la Japani (JMA). Lilihisiwa hadi Tokyo.

Waziri Mkuu Sanae Takaichi amesema serikali imeunda timu ya usimamizi wa majanga na inafanya kazi ya kutathmini athari za tetemeko la ardhi.

"Kwa wale wanaoishi katika maeneo ambayo maonyo yametolewa, tafadhali hamieni hadi maeneo ya juu na salama," Takaichi aliwaambia waandishi wa habari.

Japani ni mojawapo ya nchi zinazokumbwa na matetemeko ya ardhi zaidi duniani kwani iko katika eneo ambalo mabamba kadhaa ya tektoniki hukutana.

Inakumbwa na matetemeko ya ardhi yapatayo 1,500 kila mwaka na inakumbwa na karibu asilimia 18 ya matetemeko yote ya ardhi duniani

Tetemeko la ardhi la ukubwa wa 9 na tsunami lililopiga kaskazini mashariki mwa Japani mwaka 2011 ndio kubwa zaidi, na liliuwa watu wapatao 18,500 na kusababisha janga la nyuklia la Fukushima.