Feature Image

Ruto: Biashara Tanzania, Kenya yafikia Sh2.2 trilioni 2025 pia Maadui wa Tanzania na Kenya ni umasikini na ukosefu wa ajira

Ruto: Biashara Tanzania, Kenya yafikia Sh2.2 trilioni 2025

Rais wa Kenya, William Ruto, amesema biashara ya Tanzania na Kenya mwaka jana ilifikia Dola za Marekani 860 milioni (zaidi ya Sh2.223 trilioni).  

Ruto ameyasema hayo leo, Jumanne Mei 5, 2026 alipolihutubia Bunge la Tanzania, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini. 

Aidha amesema kuwa mataifa hayo yanategemeana ndiyo maana biashara yao mwaka 2025 ilifika Dola za Marekani milioni 860, (zaidi ya Sh2.223 trilioni.  

Hata hivyo ameeleza mwaka huu matarajio ni biashara baina ya mataifa hayo, ifikie Dola bilioni 1 (zaidi ya Sh2.6 trilioni).

 

Rais wa Kenya, William Ruto, amehimiza kuwapo kwa mshikamano mkubwa wa kikanda kati ya Tanzania na Kenya, huku akiwataja maaduia wakubwa wa nchi hizo ni umasikini na ukosefu wa ajira.

amesema tofauti kubwa za nchi hizo mbili si tofauti za kisiasa au za kitaifa, bali ni matatizo ya kijamii na kiuchumi.

Akihutubia Bungeni leo Aprili 5, 2026 jijini Dodoma, Rais Ruto amesema kwamba wananchi wa Afrika Mashariki wanapaswa kuhamisha mtazamo kutoka kwenye mgawanyiko na kuelekeza nguvu katika kushughulikia tatizo la ukosefu wa ajira na umasikini.

“Tunao maadui wengi, lakini maadui wetu si Watanzania wala Wakenya. Maadui wetu ni ukosefu wa ajira na umasikini. Kenya na Tanzania zinategemeana,” amesema Ruto katika hotuba iliyopokelewa kwa makofi na wabunge.

Hata hivyo kiongozi huyo wa Kenya amesisitiza kwamba ustawi wa Taifa moja katika eneo hili umefungamana kwa karibu na mafanikio ya majirani zake, akibainisha kuwa ushirikiano wa kiuchumi ndio msingi wa maendeleo endelevu ya Afrika Mashariki.