Kundi la mawasiliano la ulinzi la Ukraine lakutana Berlin
Kundi la mawasiliano la ulinzi la Ukraine lakutana Berlin
Kundi la Mawasiliano la Ulinzi la Ukraine linakutana hivi leo mjini Berlin kufuatia mualiko wa waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius.
Kundi la Mawasiliano la Ulinzi la Ukraine (UDCG) linakutana hivi leo mjini Berlin kwa mualiko wa Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius.
Viongozi wengine ambao pia watahudhuria kwa mazungumzo ya ana kwa ana ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Mark Rutte, Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, John Healey na Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Mykhailo Fedorov, huku washiriki wengine wakishiriki kwa njia ya video.
Mkutano huo utajadili msaada zaidi kwa Ukraine baada ya miradi mikubwa ya pande mbili kukubaliwa hapo awali na Ujerumani na Ukraine.
Aidha Ujerumani na Uingereza zilichukua uongozi wa Kundi la mawasiliano la ulinzi la Ukraine mwezi Aprili mwaka uliopita kundi hilo linazikusanya nchi zote 32 wanachama wa NATO na nchi nyingine 25, pamoja na Umoja wa Ulaya.