Feature Image

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua, amefanyiwa upasuaji

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua, amefanyiwa upasuaji kwa mafanikio baada ya kupata jeraha kubwa katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu, Pacome alipata matibabu ya haraka kabla ya kufanyiwa tathmini na jopo la madaktari wa Yanga kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Agha Khan, ambao walikubaliana kuwa afanyiwe upasuaji.

Upasuaji huo ulifanyika majira ya saa nane usiku na kukamilika salama. Sasa nyota huyo ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu kwa kipindi cha wiki sita, kabla ya kufanyiwa tathmini nyingine itakayobaini hatua ya kuanza safari ya kurejea uwanjani.