China yaonya dhidi ya mvutano, yataka Iran na Marekani warejee mezani kwa mazungumzo
China yaonya dhidi ya mvutano, yataka Iran na Marekani warejee mezani kwa mazungumzo
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China ametaka mazungumzo ya amani kati ya Iran na Marekani yaanze tena, kufuatia Marekani kuikamata meli ya mafuta ya Touska iliyokuwa na bendera ya Iran.
Guo Jiakun aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba China "ina wasiwasi" na "kukamatwa kwa nguvu" meli ya Iran na vikosi vya Marekani, kulingana na shirika la habari la AFP.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China hapo awali ilieleza kuwa hatua ya Marekani ya kuzingirwa na wanamaji kwenye bandari za Iran ni "kutowajibika na ni hatari".
China inakadiriwa kununua takriban asilimia 90 ya mafuta ya Iran yanayouzwa nje - huku wachambuzi wakisema vikwazo vya Marekani vinalenga China, ikitaka kuweka shinikizo kwa Iran.