Wagombea Uraisi Kupewa LandCruise GX VXR Mpya ya 2025 zero kilometa na INEC.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema kila mgombea atakaetimiza vigezo na kutangazwa kuwa mgombea urais wa chama cha siasa kitakacho shiriki Uchaguzi Mkuu 2025, atakabidhiwa gari maalumu kwa ajili ya kampeni.
Kwa mujibu wa INEC, wagombea hao watakabidhiwa gari aina ya LandCruise GX VXR Mpya ya 2025 zero kilometa.
Magari hayo yanatolewa kwa wagombea urais pekee, pamoja na dereva na mlinzi kwa ajili ya kumuwezesha mgombea urais kusafiri na kufika popote pale atakapohitaji kufika kwa ajili ya kurahisisha shuguli zake za kufanya Kampeni na kuomba kura kwa wananchi.
Akiwakabidhi magari hayo Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema kuwa utaratibu huo umewekwa kisheria ili kuhakilisha wagombea wote wanaendesha kampeni zao katika mazingira salama na yenye usawa.
"Utaratibu huu ni wa kisheria . Mgombea akitimiza vigezo INEC inamkabidhi gari jipya, dereva na mlinzi kwa ajili ya za kampeni," amesistiza Kailima.