Feature Image

TAARIFA MUHIMU:ZIMEBAKI SIKU 10 KABLA YA KUFUNGA DIRISHA LA MAOMBI YA MKOPO NA 'SAMIA SCHOLARSHIP' KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026

 

Zimesalia siku 10 tu! Mwisho wa kuomba Mikopo ya Elimu ya Juu na 'Samia Scholarship' unakaribia, huku dirisha la maombi likitarajiwa kufungwa kabisa tarehe 31 Agosti, 2025.

Tafadhali zingatia kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza. Kauli hii ilitolewa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari tarehe 11 Agosti, 2025.

Hivyo, kama wewe ni mwanafunzi unayehitaji msaada huu na bado haujakamilisha maombi yako, tumia fursa hii ya mwisho. Usisubiri dakika za mwisho ili kuepuka usumbufu.

Kwa msaada au taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti rasmi ya HESLB: www.heslb.go.tz, piga simu 0736 66 55 33, tuma ujumbe wa WhatsApp kupitia 0739 66 55 33 au tuma barua pepe kwenda [email protected]

Imetolewa na:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
Alhamisi, 21 Agosti 2025,

Dar es Salaam