Feature Image

SELECTION ZA VYUO VIKUU 2025/2026 ZIMETOKA!

Habari njema! Matokeo ya selection za vyuo vikuu 2025/2026 zimetoka rasmi. Jua jinsi ya kuangalia majina ya waliochaguliwa, na hatua za kufuata ili kuthibitisha nafasi yako.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa rasmi matokeo ya selection za Vyuo Vikuu kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Hii ni hatua muhimu sana kwa maelfu ya wanafunzi wanaotamani kuanza safari yao ya elimu ya juu.

Tunawapongeza kwa dhati wale wote waliochaguliwa na tunawatakia mafanikio mema katika safari yao mpya ya kitaaluma.

 

Muhimu: Ikiwa Umechaguliwa na Vyuo Zaidi ya Kimoja

Kama wewe ni miongoni mwa waliobahatika kuchaguliwa na vyuo zaidi ya kimoja (multiple selections), ni muhimu sana ufuate maagizo ya TCU ili kuthibitisha nafasi yako.

Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia leo tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2025. Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.

Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.

Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili. Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majinaya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja inapatikana kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz)

Kwa maelezo zaidi Pakua