Feature Image

MATOKEO YAMETOKA! Tazama Hapa Matokeo ya Kidato cha Pili (FTNA) na Darasa la Nne (SFNA) 2025

MATOKEO YAMETOKA! Tazama Hapa Matokeo ya Kidato cha Pili (FTNA) na Darasa la Nne (SFNA) 2025


Hatimaye kiu ya wanafunzi, wazazi, na walezi imekatwa! Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) na Darasa la Nne (SFNA).

Huu ni wakati wa furaha na tathmini kwa safari ya elimu ya watoto wetu. Kama umekuwa ukisubiri kwa hamu kujua maendeleo ya mwanao au mdogo wako, habari njema ni kwamba matokeo sasa yanapatikana kidijitali.

Jinsi ya Kuangalia Matokeo Kupitia Tovuti ya NECTA

Kuangalia matokeo ni rahisi na haraka. Fuata hatua hizi chache kulingana na matokeo unayohitaji:

1. Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Pili (FTNA)

  • Tembelea tovuti rasmi ya NECTA: www.necta.go.tz

  • Kwenye orodha ya juu (Menu), bofya sehemu iliyoandikwa "Results".

  • Chagua chaguo la "FTNA" (Form Two National Assessment).

  • Chagua mwaka husika, kisha utafute jina la shule yako kuona matokeo.

2. Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne (SFNA)

  • Tembelea tovuti ya NECTA: www.necta.go.tz

  • Bofya tab ya "Results".

  • Kwenye orodha itakayotokea, chagua "SFNA" (Standard Four National Assessment).

  • Tafuta mkoa, wilaya, na hatimaye jina la shule yako kuona alama walizopata wanafunzi.